Friday, November 7, 2014

Mrithi wa Kanumba anapika movie

Lameck Kanumba,  ambaye ni mdogo wa aliyekuwa mwigizaji nyota nchini marehemu Steven Kanumba, anatarajia kuachia filamu mpya inayokwenda kwa jina la ‘Asante Mama’

Alisema huo ni ujio wake mpya katika kuendeleza kile kilichokuwa kikifanywa na kaka yake enzi za uhai wake. Lameck alisema amepata nafasi ya kushiriki filamu hiyo iliyoandaliwa na baadhi ya wasanii waliokuwa wakifanya kazi pamoja na marehemu Kanumba, Mayasa Mrisho na Ben Branko (Serengo).
Aliongeza kuwa ana filamu hiyo imani itafanya vizuri sokoni na hivyo kuwa katika mstari mzuri wa kusonga mbele katika tasnia ya filamu nchini Tanzania.

Shetta alia na Collabo za Nje, anataka kufuata nyayo za Diamond

Msanii ambaye kiribu nyimbo zake zote ameshirikisha wasanii wengine Shetta ambaye kwa sasa amesema hana mpango wakufanya kazi tena na wasanii wa hapa Shetta aliongea hayo alipo ulizwa kupitia Power Jams ya EA Radio kama anampango wakufanya kazi na Ally Kiba Shetta alijibu “Sina mpango wakufanya collabo na Ally Kiba”“Nafikiria zaidi kufanya Collabo International kwa sababu nimesha fanya kazi nyingi sana na wasanii wa nyumbani nazani sasa inatosha aidha nifanye nyimbo mwenyewe au nifanye na International artist.”

Picha: Waje na Diamond washoot video jijini Cape Town, SA

Diamond Platnumz ameamua kusafiri hadi jijini Cape Town, Afrika Kusini kwenda kushoot video ya wimbo alioshirikishwa na msanii wa Nigeria, Waje. Diamond na Waje Video hiyo imefanyika kakita fukwe za bahari ya Atlantic jijini Cape TownTazama Picha hapa....Shilole: Muziki dili kuliko movie,

Msanii wa muziki wa kizazi kipya na muigizaji wa movie, Shilole au jina halisi Zuwena Mohamed amedai kuwa muziki ndio unaompa jeuri la kula bata mtaani.Shilole aliyetamba na tracks kama Nakomaa na Jiji na Chuna Buzi, amesema kuwa muziki ndiyo unaomfanya aonekane mrembo na kutanua mtaani kwa kuwa unamwingizia fedha nyingi kuliko anazozipata katika movie.

Msanii huyo aliyedai kwa sasa yuko jikoni anaandaa ngoma ya kufunga mwaka itakayoingia sokoni mwezi ujao, alisema ameamua kuweka kando uigizaji kwa muda ili akusanye fedha kwenye muziki ili baadaye aweze kutengeneza movie yake.
ADVERTISEMENT